Bado klabu ya Yanga, imezidi kuweka mkazo katika kumuhitaji nahodha wa Taifa Stars, na klabu ya Azam Himid Mao ikimuhitaji kabla ya kuanza kwa ligi Klabu ya Yanga inapambana kuhakikisha kuhakikisha inaipata saini ya kiungo mkabaji wa Azam FC, Himid Mao ambaye anaelekea kumaliza mkataba wake na miamba hiyo ya Tanzania Bara.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa Yanga Husseni Nyika ameiambia Goal, wanamuhitaji mchezaji huyo na tayari wameshaanza mazungumzo na timu yake kuona namna gani wanaweza kumchukua kabla ya pazia la dirisha la usajili kufungwa.

“Nimchezaji ambaye tunamuhitaji kweli kweli, kutokana na michuano inayotukabili huko mbele ya safari na ukweli tumeshapeleka ujumbe kwa uongozi wa Azam kuona ninamna gani wanaweza kutuuzia mchezaji huyo,”amesema Nyika.
Kiongozi huyo amesema Azam haina mashindano yoyote msimu unaokuja hivyo nivyema wakaacha kuwaekea vikwazo katika biashara hiyo na kuridhia usajili huo ili Mao akipige Jangwani msimu ujao.

“Mchezaji mwenye yupo tayari kuondoka Azam tatizo ni klabu yake imekuwa na mambo mengi lakini bado hatujakata tamaa tutaendelea kuongea nao kuona tutaishia wapi tunachotaka ni kukimbizana na muda ka
bla dirisha la usajili halijafungwa,”amesema Nyika. Mbali na Mao pia kuna habari kwamba klabu hiyo inataka kumrudisha na Mrisho Ngasa na usajili wa wawili hao utatangazwa rasmi siku ya mwisho ya usajili Agosti 6.

Post a Comment

 
Top