Figisutz inapenda kukuletea makala ya wachezaji kinda watakaotisha Ligi Kuu Bara msimu ujao iwapo watapata fursa ya kucheza kwenye klabu zao
Kuna kundi kubwa la wachezaji chipukizi wanaotarajiwa kuwa moto wa kuotea mbali msimu ujao, baada ya badhi yao kuanza kuonesha dalili msimu uliopita na mashindano mbali mbali.
Endapo klabu zitawaamini na kuwapa nafasi mara kwa mara, wanaweza kuwa na msaada ndani ya timu kwani wana sifa zote za kuwa wachezaji wakubwa katika mpira wa miguu.
figisutz inakuletea baadhi ya wachezaji chipukizi wanaotarajiwa kutamba msimu ujao wa Ligi Kuu Bara kama wakipata nafasi za mara kwa mara.
Shaabani Idd
Zao kutoka klabu ya Azam, mfungaji bora wa michuano ya U-20 msimu uliopita, mshambuliaji huyo msimu uliomalizika Ligi Kuu alifanikiwa kufunga magoli 7 mawili nyuma ya kinara wa magoli wa klabu ya Azam, John Bocco.
Eliud David
Hakupata mechi nyingi sana msimu uliomalizika, ila mechi chache alizopewa na mwalimu Kinnah Phiri zilitosha kujitambulisha mbele ya kocha huyo raia wa Malawi, Eliud msimu ujao anatazamiwa kupata nafasi ya kutosha kikosi cha kwanza Mbeya City.
George Sangija
Kiungo mshambuliaji wa Mbao FC ya Mwanza, Sangija alimaliza na magoli mawili na kutoa pasi mbili za magoli dhidi ya Simba na Yanga, chipukizi huyo ana uwezo mkubwa wa kumiliki mpira na kutengeneza pasi za mwisho.
Masoud Abdallah
Kiungo mshambuliaji wa Azam, kinda huyo anatarajiwa kuwa zao la klabu kwa miaka ijayo, uwezo wake mkubwa wa kusakata kabumbu unatarajiwa kumpa nafasi ya kutosha kwa msimu ujao.
Yusuph Mhilu
Amekuwa ndani ya klabu ya Yanga kwa Msimu wa tatu mfululizo na kufanya vizuri kila anapopata nafasi, msimu ujao anatazamiwa kupata mechi nyingi kuliko misimu ya nyuma.
Bakari Masoud
Kiungo bora wa kizazi chake hapa nchini, nyota huyo wa Simba anatarajiwa kufanya makubwa Msimu ujao kama benchi la ufundi chini ya mwalimu Omog litamuamini na kumpa nafasi.
Kelvin Naftal
Kinda wa Serengeti Boys na klabu ya RUVU Shooting, Naftal tayari amesha cheza kwenye baadhi ya mechi za Ligi Kuu msimu uliopita.
Maka Edward
Japo siyo jambo jepesi kupata nafasi ndani ya Yanga kwenye eneo la kiungo, ila Maka ni mmoja wa kiungo bora kwa umri wake endapo akipewa muda atafanya
Post a Comment