14.6.2017
Kitaifa
1. Kishindo chaendelea Msimbazi: John Bocco nae katambulishwa Rasmi Simba. Kasaini miaka miwili.

2. Kizungumkuti: Baraza la michezo BMT lapiga stop Uchaguzi TFF. Lasema halijapewa taarifa.

3. Naodha wa Serengeti boys aliyeumia akiwa Gabon, Issa makamba akana kutelekezwa na TFF.

4. Imedaiwa kinachoipa Simba jeuri kunako Usajili ni fungu alilotoa mohamed Dewji 'Mo'.

5. Klabu ya Yanga yajinasibu haisajili kufuata Upepo. Katibu mkuu, Mkwasa asema wanazingatia Ripoti ya benchi la Ufundi.

6. Kwenye usajili
-imedaiwa Kichuya sasa kumuachia Okwi jez na 25.

-imedaiwa winga wa Mbao, Pius Buswita hakusaini Yanga bali Simba SC.

-imedokezwa Niyonzima kakubaliana na simba na sasa yu mbioni kutambulishwa.

-Himid mao mbioni kuvunja mkataba Azam atimkie kwingine.

-imedokezwa Bossou kama Donald Ngoma, nae sasa kutimka jumla jumla Yanga SC.

-imedaiwa milion 130 zimetolewa kiwabakiza Ajib, Banda klabuni Simba.

-Imedokezwa Mkude nae mambo safi, uwezekano wa kubaki Simba waanza kuonekana.

-Eric Ngwegwe sasa mbioni kurejeshwa kikosini Mbao FC.

Kimataifa
1. Cheikh Tiote aagwa huko Beijing.

2. Matokeo mechi za kirafiki
-Ufaransa 3 Uingereza 2
(Umtiti,Sidibe, Ousmane Dembele)
(Harry Kane, Harry Kane).

-Afrika Kusini 1 - 2 Zambia.

-Romania 3 - 2 Chile
(Stancu, Stanciu, Baluta)
(E.Vargas, L.Valencia)

-Cameroon 0 - 4 Colombia
(James,Mina,Mina,Izquierdo)

-Norway 1 - 1 Sweden
(Elyounoussi, Armentoros)

-Australia 0 - 4 Brazil
(Diego Souza,Thiago Silva,Taisan,Diego Souza)

-Singapore 0 - 6 Argentina
(Fazio, Correa, Gomez,Paredes,Alario, Di Maria)

Hong Kong 1 - 1 Korea Kaskazini.

3. Ronaldo nae kikaangoni Hispania. Kashitakiwa kwa kukwepa kodi.

4. Imethibitishwa kweli Griezmann kaongeza mwaka mmoja mpk 2022, aomba radhi kuhusu kauli yake ya uwezekano wa kutua man utd kuwa 6/10.

5. Kwenye Usajili.
-As Roma yapata kocha mpya anaitwa Eusébio Di Francesco. Alikuwa Sassuolo.

-aliyekuwa kocha wa AS Roma,Luciano Spalleti alitimkia Inter Milan.

-imedaiwa Claudio Ranieri katua FC Nantes ya Ufaransa.

-Mathieu Valbuena katoka Olympic lyon katua fernebahce kwa dau la pauni mil 1.3.

-Olympique Lyon sasa inahusishwa na Bertrand Traore.

-imedaiwa David Ospina pia kakarbia kutua Fernebahce.

-imedaiwa Alexandre Lacazate huenda akaigharimu Arsenal pauni mil 60.

-Arsenal, West Ham zadaiwa kuangalia uwezekano wa kumnasa Chris Smalling.

-Juventus yaingia anga za Arsenal, Barcelona. Inahusishwa na Mahrez.

-Everton yakubaliana na Sunderland uhamisho wa mlinda lango, Pickford, pauni mil 30.

-Everton yaendelea na mazungumzo kuhusu uwezekano wa kumnasa Klassen wa Ajax.

-West Brom nayo yahusishwa na John Terry (JT).

-man City sasa kuanza mazngmzo Rasmi na Kyle Walker.

-Chelsea, man utd zamgombea winga wa Fiorentina, Federico Bernadeshi.

-Schweinsteiger akana uwezekano wa kutua tena Bundesliga kwasasa asema ana furaha Amerika.

6. Tumalize na vijimambo, vijineno na Povu.
-Manchester Utd inaamini itamnasa Ivan Perisic toka Inter Milan.

-aliyekuwa mlinda lango wa Man City, Wily Cabarelo sasa anukia Chelsea.

-Marco Ansensio mbiob kusain mkataba mpya Madrid utaokuwa na kipengele chá dau la pauni mil 308 kama ada ya uhamisho.

-jarida la Manchester Evening news, ladai man Utd inamtaka Nemanja Matic na sio Fabinho.

-nao Adidas huenda wakatibua dili la James kwenda Man Utd. Imedaiwa ana mkataba utaohitaji avae jezi namba 10 inayovaliwa nae Wayne Rooney ambae angali na mkataba wa miaka mitatu.

Post a Comment

 
Top