13.6.2017
Tuanze na ilonifikia hivi punde kutoka kwenye mpira wa Kikapu: The Golden State Warriors imetwaa Taji lake la Pili la NBA ndani ya miaka mitatu....
-Cavariels kakalishwa 129-120..
-Kevin  Durant kaweka point 39, rebound 7 na assist 5.
-Le Bron James akiweka point 41, rebound 13 na Assist 8.
-Durant pia katangazwa kuwa MVP.

Kitaifa:
1. Sio tetesi tena: Shomari Kapombe arejea Rasmi simba.

2. Stars kuingia kambin juni 14 kujiandaa na michuano ya Cosafa.
-Kikosi kutajwa leo.

3. Uchaguzi TFF pale pale
-unafanyika Agosti 12
-Tume yaonya Rushwa na yasiyofaa
-fomu kuchukuliwa Juni 16 mpk 20
-mchujo ni juni 21-23
-uzoefu miaka mitano.

4. Kwenye sakasaka za usajili
-imedaiwa Yanga imemnasa Buswita toka Mbao FC.

-imedaiwa Azam sasa imemgeukia Salum Kimenya amrithi Kapombe.

-Singida, Mtibwa, mbeya city zahusishwa na mlinda lango mwingube wa Mbao, Emmanuel Mseja.

-Singida utd yahusishwa na mlinda lango wa Serengeti boys, Ramadhan Kabwili.

-kuwasili kwa Manula, Kapombe kwazua habari ya Agyei, Bokungu bye bye Simba.

-imedaiwa Niyonzima kakana kuwa mbioni kutua Simba.

-Mbonde wa Mtibwa asema bado anatafakari kabla hajaamua kutimkia Vilabu vya kariakoo.

-imedaiwa Simba sasa yahaha kuwabakiza James Kotei, Mkude, Ajib.

-Kaseja huenda akabaki zake Kagera Sugar.

Kimataifa
-Iran yaungana na Urusi, na Brazil kufuzu kombe la dunia 2018.
-imeifunga Uzbekistan 2-0.

2. Mlinda lango wa Juventus, Gianluig Buffon asema msimu ni wa mwisho kwake.

3. Tukigeukia usajili..
-André Silva katoka Porto katua AC Milan.

-Fabio Capello nae katua China.

-Real Madrid mbioni kumrudsha Jesus Vallejo Bernabeu. Alikuwa kwa mkopo Eintranch Frankfurt.

-Barcelona yamtangea paun mil 100 kiungo wa PSG, Marco verrati.

-nyingine yadau Verrati Kaomba kuondoka Psg.

-Juventus huenda ikaipiku Arsenal kwa Mahrez.

-imedaiwa Psg inakaribia kumnasa mbappe.

-Man City yatajwa kuafikia na Alexis Sanchez.

-Chelsea sasa yamgeukia Lorenzo Insigne wa Napoli kama mbadala wa Eden hazard endapo ataondoka.

-John Terry sasa ahusishwa na Aston Villa.

-Ross Barkerly agomea mshahara wa paun 100,000 kwa wiki Everton.

-Everton yakaribia kumnasa Sandro Ramirez toka Malaga.

-Renato Sanchez kuitosa tena Man utd na kubaki Bayern.

-Bayern pia yaripotiwa kukaribia kumnasa Tolisso wa Lyon.

-Liverpool nayo yajitosa kumuwania Kylian mbappe.

-Liverpool pia yatajwa kufufua harakati za kumnasa Mohamed Salah.

-Januzaj sasa kuuzwa kwa pauni mil 10 pekee.

-nae Diego Costa kasema anangojea Chelsea waamue hatma yake.

4. Tumalize na vijimambo, vijineno na Povu.
-Wakala wa Morata asema ofa ya Man Utd imepokelewa ila bado haijajibiwa na Real Madrid.

-kiungo wa zaman wa Manchester United aitwaye Ray Wilkins asema Lindelof bora man utd ingemnasa Michael Keane.

-aliyepata kuwa kocha wa Bayern, Jupp Heynckes asema Toni Kroos hata akistaafu soka ni sawa tu. Asema kuwa na miaka 27 ukatwaa mataji aliyoishabeba hakuna alichobakiza.

-nalo jarida la The marca lafichua na kudai Griezmann kaongeza mkataba Atlético Madrid mpk 2022.

Post a Comment

 
Top