Klabu ya Simba kwa sasa inapambana kuwasajili Haruna Niyonzima na Simon Msuva, lakini Daniel Agyei na Manyika Peter wametupiwa virago vyao
Aliyekuwa kipa chaguo la kwanza wa Simba Mghana Daniel Agyei, ametemwa kwenye kikosi cha timu hiyo cha msimu ujao baada ya kusajiliwa kwa Aishi Manula na msaidizi wake Emmanuel Mseja.
Kocha msaidizi wa Simba Jackson Mayanja amfigisutz, kuwa msimu ujao goli lao litalindwa na makipa wapya ambao Manula na Mseja walisajiliwa hivi karibuni .
“Haya ni mabadiliko ya kawaida ambayo hufanywa na timu yoyote duniani kwaiyo tunamshukuru sana Agyei na Manyika Peter kwa mchango wao naamini kwa uwezo waliokuwa nao wanaweza kupata timu ya kucheza,” amesema Mayanja.
Kocha huyo ambaye kwa sasa yupo mapumzikoni Uganda amesema kwa kikosi kilichopo hivi sasa ana matumaini makubwa ya kuiona timu hiyo ikifanya vizuri kwenye michuano yote watakayoshiriki ikiwemo ile ya kimataifa.
Amesema kwa usajili huo haoni wao kama makocha wamekosea mahali, endapo watakosa ubingwa wao ndiyo wanapaswa kulaumiwa kutokana na timu hiyo kukusanya wachezaji wote bora nchini.
“Nadhani msimu ujao utakuwa mwaka wa Simba sioni kama kutakuwa na timu ambayo inaweza kutusumbua kiasi cha kuhofia kukosa ubingwa kama ilivyokuwa siku za nyuma tumesajili wachezaji wenye ubora wa hali ya juu lakini pia wazoefu wa mambo yaha,” amesema.
Wachezaji ambao tayari wamesaini kuichezea Simba msimu ujao ni John Bocco, Aishi Manula, Shomari Kapombe, Mseja na Jamali Mwambeleko.
Simba kwa sasa inapambana kuhakikisha inawasajili wachezaji wawili wa Yanga ambao ni kiungo wa kimataifa kutoka Rwanda Haruna Niyonzmia na mfungaji
Post a Comment