Tayari ratiba ya michuano mipya ya Kombe la Sportpesa imeshatoka. Michuano hio inashirikisha timu nane za Simba, Yanga na Singida United kwa upande wa Tanzania Bara huku Jang’ombe ikiwakilisha visiwa vya Zanzibar.

Kenya watawakilishwa na timu nne za Gor Mahia, AFC Lepoards, Nakuru All Stars na Tusker. Mechi mbili zitpigwa kwa siku huku hatua ya nusu fainali ikitarajiwa kucheza tarehe 8 mwezi wa sita na fainali tarehe 11 mwezi wa sita jijini Dar.

Post a Comment

 
Top