WAKATI mabosi wa Simba wakikuna
kichwa jinsi ya kumalizana na wachezaji
wao juu ya malimbikizo ya mishahara ya
miezi miwili, aliyekuwa Kocha Mkuu wa
timu hiyo, Zdravkov Lugarusic ‘Loga’
ameibuka tena Msimbazi kivingine.
Kocha huyo kutoka Croatia ametishia
kuiburuza klabu hiyo Fifa akitaka alipwe
karibu Dola 40,000 (zaidi ya Sh 80 Milioni)
kwa kuvunjiwa mkataba na klabu hiyo.
Loga aliyewahi kuinoa AFC Leopards ya
Kenya, kupitia Kampuni ya Uwakili ya
Mwambilianga, Majani &Associates
amewasilisha barua klabu ya Simba
iliyopokewa Jumatano ya wiki hii, akitoa
siku 10 ili Simba imlipe chake.
Katika barua hiyo ya Novemba 8,
iliyotumwa kwa Rais wa Simba, Evans
Aveva imedai kuwa mabosi hao wa
zamani wawe wameshamlipa fedha hizo
la sivyo atawaburuza Fifa kudai haki yake
kwa kuvunjiwa mkataba kabla
haujamalizika.
Loga anataka alipwe Dola 38,293.50. kwa
kusitishiwa mkataba ulioanza Julai 15,
2014 hadi Mei 30, 2015, lakini ukavunjwa
Agosti, 2014 baada ya kipigo cha mabao
3-0 toka kwa Zesco katika mechi ya Simba
Day.
Mchanganuo wa fidia hiyo ni Dola 6,000
( Sh 12 milioni) za usumbufu wa
kuvunjiwa mkataba waliokubaliana
wakati wakisaini mkataba huo kuwa
pande itakayovunja imlipe mwenzie, pia
mshahara wa miezi 10 tangu avunjiwe
mkataba ambao ni sawa Dola 30,000
(alikuwa akilipwa kwa mwezi Dola 3,000),
huku marupurupu mengine ya Dola
2,293.15 posho ya usafiri na intaneti kwa
miezi 10.
Uongozi wa Simba kupitia Katibu Mkuu
wake, Patrick Kahemele alikiri kupokea
notisi hiyo ya Loga na kusema uongozi
ungekaa kupitia mkataba wake kwa
sababu wakati hayo yakitokea Simba
ilikuwa ikiongozwa na wengine.
“Kweli barua hiyo imepokewa tunaangalia
jinsi ya kuifanyia kazi, lazima
tujiridhishwe kwa kila kilichoainisha na
kuchukua maamuzi ni suala la muda wa
siku 10 tuliopewa,” alisema.
Notisi ya Loga imekuja miezi kadhaa
baada ya Simba kulazimishwa na Fifa
kumlipa aliyekuwa beki wao, Donald
Mosoti ambaye kesi yake ilisimamiwa pia
na kampuni inayomsimamia sasa Loga
ambaye kwa sasa anainoa Inter Clube ya
Angola.
MISHAHARA
Katika hatua nyingine Kahemele amekiri
kuwa ni kweli nyota wa Simba wanadai
mishahara ya miezi miwili ya Septemba
na Oktoba.
Kahemele alitoa ufafanuzi huo baada ya
kuulizwa juu ya ukweli kwamba nyota
wao wamekuwa kwenye mgomo baridi
kushinikiza kulipwa malimbikizo ya
mishahara ya miezi mitatu. Simba
ilipoteza mechi mbili za ligi mfululizo
dhidi ya African Lyon na Prisons.
“Tunadaiwa miezi miwili tu na
tunapambana ili kuwalipa, kuhusu fedha
za MO, Mohammed Dewji ni kweli alilipa
mara moja, lakini fahamu Simba ina
madeni kila kona, ila wachezaji watalipwa
fedha zao kwani ni haki yao,” alisema
Kahamele.

DODONDOSHA COMMENT YAKO

Post a Comment

 
Top