Rais wa klabu ya Simba Evans Aveva, amesema watafanya kila linalowezekana kuhakikisha timu hiyo inabeba ubingwa wa Ligi ya Vodacom msimu huu.
Aveva ameiambia Goal , ili hilo liweze kutimia wamepanga kumtimizia mahitaji yote kocha wao Joseph Omog, ikiwepo fedha za kusajili mchezaji anayemtaka katika kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili.
“Ukweli Simba ni timu kubwa kukaa misimi minne bila tajilolote, ni kushusha hadhi ya klabu ndiyo maana tumejipanga kuhakikisha kwa hali yoyote Simba inakuwa bingwa msimu huu.
Rais huyo ambaye amekuwa na wakati mgumu kwa kushindwa kubeba taji lolote tangu aingie madarkani Julai 2014, amesema kwasasa wamepanga kumrudisha nchini mshambuliaji wa Kiganda Emmanuel Okwi , anayeichezea klabu ya Sonderjiske ya Denmark.
Amesema baada ya hapo watasikiliza ripoti ya kocha wao Omog, inasemaje baada ya kumalizika kwa mzunguko wa kwanza na endapo itamuhitaji mchezaji yeyote kutoka timu yoyote Afrika Mashariki na kati na hata Magharibi na Kaskazini wapo tayari kufanya hivyo ili kutimiza lengo lao la ubingwa.
“Unajua unapotaka mafanikio lazima uwe na bajeti kubwa na kikosi kizuri chenye ushindani ndicho tunachotaka sisi Simba kwasababu tumechoka kuwa wasindikizaji tunachotaka ni kurudisha heshima yetu kwa kutwaa ubingwa wa Vodacom na kushiriki michuano ya kimataifa,”amesema Aveva.
Kiongozi huyo amesema anajua vikwzo vikovingi mbele yao lakini watajitahidi kupambana navyo na kuhakikisha wanatimiza kile walichokikusudia ambacho ni ubingwa msimu huu.
Aveva licha ya kuingia madarakani kwa mbwembwe nyingi lakini ameshindwa kutimiza ndoto za mashabiki na wanachama wa timu hiyo kutokana na kushindwa kuipa mafanikio na tayari amebaki miezi michache kabla ya kumaliza muda wake wa miaka minne ili aondoke madarakani
Post a Comment