Katika jangwa la Sahara, siafu wanatakiwa kusafiri jangwani kutafuta wadudu waliokufa ambao ni chakula chao. Jangwani kuna joto kali sana, inawabidi siafu hao warudi nyumbani kwa kasi ili wasife njiani.
Utafiti wa zamani umethibitisha kuwa siafu wanarekodi hatua zao ili kupima umbali waliosafiri. Na ripoti mpya iliyotolewa kwenye tovuti ya gazeti la Sayansi inaonesha kuwa si kama tu wanapima umbali kwa kurekodi hatua zao, bali pia kwa macho yao. Njia yao ya kupima umbali ni kama tunavyokadiri umbali na mwelekeo kwa macho yetu tunapokuwa garini.
Watafiti waliyafunika macho ya siafu kwa rangi ya njano, ili kujua kama wanaweza kurudi nyumbani au la bila kuona. Matokeo yanaonesha kuwa, siafu wanaotembea kwa miguu yao wanaweza kurudi nyumbani bila kuona, lakini siafu wafanyakazi waliokwenda mbali kwa kubebwa na siafu wengine hawawezi kurudi. Kama macho yao hayajafunikwa, basi ingawa hawajui siafu waliowabeba walitembea kwa hatua ngapi, bado wanaweza kurudi nyumbani kwa kupima umbali kwa macho yao. Hili ni jambo la kushangaza, kwani kabla ya hapo wanasayansi walifikiri macho yao hayawasaidii sana.
Watafiti walisema mazingira ya siafu hao ni magumu sana, inawabidi kujifunza njia mbili za kupima umbali, yaani kuhesabu hatua na kuona.
Home
»
»Unlabelled
» #SayansiNaTeknolojia Siafu wanajuaje njia ya kurudi nyumbani?
Recent Posts
- IBRAHIM AJIBU,RAFAEL DAUD NA GADIEL MICHAEL WATOWEKA KAMBINI YANGA MJINI MOROGORO26 Apr 20180
Wakati Yanga wakiwa kambini mjini morogoro wakijiandaa na mchezo wao muhimu wa ligi kuu dhidi ya mt...Read more »
- YANGA KUWAKOSA NYOTA WAKE WANNE IKIWAVAA YA WELAYTA DICHA JUMAMOSI HII04 Apr 20180
Wakati zikiwa zimesalia siku kadhaa kuelekea mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika, Yanga itawakosa w...Read more »
- MAZEMBE WAMEANZA HARAKATI ZA KUMSAJILI SHIZA KICHUYA.31 Mar 20180
Taarifa zinaeleza kuwa Uongozi wa klabu ya TP Mazembe inayoshiriki Ligi Kuu nchini Congo umeanza har...Read more »
- Droo ya robo fainali UEFA Champions League16 Mar 20180
Droo ya robo fainali UEFA Champions League Barcelona v Roma Sevilla v Bayern Munich Juventus v Real...Read more »
- Draw ya Uefa Champions league sasa IPO wazi16 Mar 20180
Draw ya Uefa Champions league sasa IPO wazi Ratiba ya Uefa Champions league imetangazwa Leo hi...Read more »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.