Baadhi ya wachumi nchini wametofautiana kuhusu kauli ya Rais John Magufuli kutishia kubadili fedha ili kuwadhibiti watu wenye tabia ya kuzificha, huku Gavana wa Benki Kuu Tanzania (BoT), Profesa Benno Ndullu akisema kauli ya kiongozi mkuu huyo wa nchi inajitosheleza na hawezi kutoa tafsiri yoyote.

Wakati Profesa wa Uchumi, Chuo Kikuu cha Mzumbe, Honest Ngowi akisema haamini kama fedha zilizofichwa ni nyingi kiasi cha kuteteresha mzunguko wa fedha nchini na kutaka zitizamwe sababu za fedha kutoonekana, Mhadhiri wa Chuo Kikuu Huria (OUT) mkoani Iringa, Dk Bukaza Chachage alisema kuficha fedha kwa nia ovu ni kosa kubwa kwa sababu huhatarisha uchumi wa nchi.
Source:mwananchi

Post a Comment

 
Top