USHINDI wa mabao 5-0 walioupata Simba jana dhidi ya Hard Rock ya visiwani Zanzibar ulifunikwa na ubora wa mabao mawili yaliyofungwa na viungo Said Ndemla na Mwinyi Kazimoto huku lile la Ndemla likiacha gumzo kubwa zaidi.

Ndemla alipokea mpira akiwa jirani na walinzi wawili wa Hard Rock ambapo alifanikiwa kumtoroka mmoja huku akimfuata mwingine

Wakati akimkaribia mlinzi wa pili, Ndemla alibadili uelekeo ghafla kitendo kilichosababisha beki huyo ateleze na kuanguka

Baada ya kufanikisha azma hiyo, Ndemla aliongeza kasi akiingia kati eneo la usawa wa goli

Walinzi wa Hard Rock walichelewa kumfikia kabla hajaachia shuti kali lililojaa wavuni moja kwa moja

Laudit Mavugo akimpongeza Ndemla baada ya bao hilo.

Post a Comment

 
Top