SIMBA SC
1. Aishi Manula
Ameonesha kiwango kizuri hususani kwenye mikwaju ya penati baada ya kuokoa penati ya Kelvin Yondani. Ndani ya dakika 90 hakupata kashi kashi sana kutokana na ubutu wa safu ya ushambuliaji ya Yanga SC leo . Anapata alama 7/10
2. Ally Shomari
Ni derby yake ya kwanza lakini ameonesha utulivu mkubwa kwenye marking na kupandisha mashambulizi. Nidhamu ya ukabaji na uelewano mzuri na wenzake ilikuwa silaha nzuri kuwazuia Yanga wing ya kushoto alipokuwepo Emanuel Martin na Gadiel chini yake . Anapata alama 6/10
3. Erasto Nyoni
Uzoefu na ukongwe kwenye soka vimemsaidia sana leo . Mara nyingi alikuwa akipanda juu kuongeza kasi na kuingia eneo la kati kusaidia kukaba na kusukuma mipira mbele kwa pasi ndefu . Hakuwa aggressive sana kwenye wing kama alivyozoeleka. Anapata alama 5/10
4. Salim Bonde
Alikuwa makini kwenye mipira ya juu . Mara nyingi mwenzake Mwanjali alionesha kupaniki lakini Mbonde alikuwa akisahihisha makos yake . Alishirikiana vyema na kiungo wa chini James Kotei kuua driving force Yanga njia ya kati kwa Tshishimbi, Kamusoko na Donald Ngoma . Anapata alama 7/10.
5. Method Mwanjali
Sweeper wa Simba leo . Alisimama kuhakikisha lango lao lipo makini na ku ' command ' walinzi wengine kuwa makini muda wote . Paniki na jazba kwa nyakati fulani zilitaka kumtoa mchezoni . Alipata kqdi ya njano kwa hilo . Bado ni muhimili kwa Simba eneo la kati . Anapata alama 5/10
6. James Kotei
Sikuelewa kwanini Joseph Omog alimwacha acheze dakika zote 90. Hakulimudu vyema eneo la kiungo cha chini kama ambavyo Jonasi Mkude hufanya . Ubora wa Haruna Niyonzima eneo hilo ambaye alikuwa akishuka na kupanda chini sanjari na Mzamiru Yassin ulificha makosa yake . Alikuwa mzuri kukaba kwa kiasi lakini hakujenga mfumo mzuri wa mashambulizi tokea kati hivyo kujikuta Simba inamiliki vyema mpira lakini kwenda mbele ni shida. Anapata 5/10
7. Shiza Kichuya
Kama sio goli lake zuri kwenye mikwaju ya penati asingekumbukwa sana kwenye mechi ya leo kama ilivyo kawaida yake . Hakuweza kuisadia Simba kujenga mashambulizi makali kutokea kwake . Muda mwingi alionekana kudhibitiwa vyema na mlinzi wa kushoto wa Yanga Gadiel Mbaga . Licha yakuwa chaguo la mwalimu kupiga mipira iliyokufa hususani kona, lakini hakuweza kutengeneza goli. Uzuri kwake ni kusaidia kukaba na kumfanyia screening Haruna Niyonzima aliyekuwa anahaha eneo lote la kiungo. Anapata alama 4/10.
8. Mzamiru Yassin
Wengi wanaweza kuhisi game ya leo ilimkataa kiungo huyu ambaye msimu uliopita aliibeba sana Simba eneo la kiungo. Mfumo wa uchezaji wa Haruna Niyonzima ndio uliomfanya Mzamiru asionekane uwanjani kama kiungo mchezeshaji eneo la juu. Huyu aligundua majukumu hayo Haruna kayashikiria vyema hivyo yeye kushuka chini kidogo kumsaidia Kotei kuimarisha kiungo cha chini ingawa kwa upande wa kushoto baada ya Haruna kucheza kama kiungo huru. Kuna wakati alikuwa akijaribu kukunjuka kama invisible attacking midfielder lakini muunganiko wa Tshishimbi na Kamusoko eneo la kati ulimfanya kuwa makini kwenye marking zaidi. Kocha alimtoa kipindi cha pili kumleta MO Ibrahimu achukue nafasi yake baada ya kuona Yanga wameanza kupwaya kwenye kiungo na alihitaji mtu wa kutembeza mpira mbele . Anapata 6/10.
9. Laudit Mavugo
Kufa kwa wing ya kushoto baada ya Haruna kucheza kama kiungo huru na Mzamiru muda mwingi kucheza chini ya box huku Kichuya kubanwa na Gadiel Michael, kulimfanya mshambuliaji huyu wa kati kushindwa muda mwingi kusimama eneo la mbele ambalo mipira mizuri ya mwisho ilikuwa hamfikii zaidi ya free header mbili alizopiga . Muda mwingi alikuwa akirudi chini kutafuta mpira au kupokea kutokana na mfumo wa give and go ambao Simba walikuwa wakicheza . Hakuwa na mbinu nyingi kuupita ukuta wa Yanga wa Yondani na Dante ukisaidia vyema Mbaga . Alitolewa na kuingia Luizio kucheza kama tisa kamili wa kusimama mbele . Anapata 4/10
10. Emanuel Okwi
Hakuwa bora sana kama wengi wanavyomjua Emanuel Okwi . Yanga walimjua atakuwa mpishi wa mwisho wa Simba kwenye final third hivyo mara nyingi hawakuruhu kuwa huru eneo lao. Tshishimbi, Kamusoko na Gadiel Michael aliyekuwa akihaha eneo lote la ulinzi walikuwa wanamtibulia mara kwa mara . Waliukataa muunganiko wake na Haruna Niyonzima. Penati yake bora inampa credit kama godfather wa team . Anapata 6/10.
11. Haruna Niyonzima
Ni bahati na umakini wa safu za kiungo na ulinzi za Yanga SC zilimzuia kiungo huyu kuifanya Simba SC isimalize mchezo ndani ya dakika 90. Ni kama aliubeba mfumo mzima wa kushambulia wa timu hiyo mabegani mwake. Aliweza kuwalazimisha Yanga mara kwa mara kurudi nyuma kuhakikisha mstari wa ulinzi upo makini. Aliweza kutengeneza nafasi 2 za wazi kwa Mavugo na Okwi kufunga lakini umakini ukawa mdogo. Dakika ya 78 almanusura aipatia Simba goli lakini alipaisha juu. Ubora wa penati yake unambeba pia. Huyu ndio man of the match kwa Simba . Anapata 9/10
YANGA SC
1. Youthe Rostand
Bila shaka anakwenda kuwa muhimili kamili langoni mwa Yanga SC . Muda mwingi ameonesha utulivu langoni na ukali pia kwa makosa ya Dante na Yondani ambao kwa kiasi walikuwa wanakati kwenye marking ya mipira ya juu. Hakupata tabu sana ya mashambulizi kutokana na ubutu wa safu ya ushambuliaji ya Simba . Kudaka penati kunampa credit kwenye derby yake ya kwanza . Anapata alama 7/10.
2. Juma Abdul
Alitimiza vyema majukumu yake ya ulinzi. Mara kwa mara aliweza kumzuia Emanuel Okwi aliyekuwa akijaribu kutanulia upande wake ili kushambulia kutokea pembeni au kupiga krosi .Rafu mbaya iliweza kumpa kadi ya njano na alitoka nje dakika tano kabla ya mchezo kuisha. Anapata 6/10.
3. Gadiel Michael
Ni dhahiri Haji Mwinyi ana kazi ya ziada kuichukua namba yake kwa mlinzi huyu wa kushoto . Huyu leo ndio kwa asilimia kubwa amewanyima Simba ushindi . Licha ya kupangwa kama mlinzi wa kushoto , aligundua mapema kukatika kwa walinzi wa kati hivyo akawa anaingia kusaidia marking. Ni zaidi ya clear chances mbili mpaka tatu za Simba kufunga aliweza kuziua . Ni mechi yake ya kwanza na kikosi cha Yanga lakini ameonesha uwezo mkubwa hata kwenye kupandisha mashambulizi. Anapata alama 9/10.
4. Andrew Vicent
Kama ilivyo ada aliendelea kuonesha ubora wake kwenye mipira ya juu lakini bado umakini kwenye pre-marking. Yaani kumkaba mtu kabla ya mpira haujamfikia. Zaidi ya mara mbili alifokewa na Rostand kumwacha Mavugo kupiga kichwa huru . Muunganiko wake na Yondani bado sio mzuri baada ya kujikuta wanakosa mtu wa mwisho kubaki mwenzake akifata mpira . Makosa yao mengi yalifutwa na Tshishimbi na Gadiel Michael. Anapata alama 5/10.
5. Kelvin Yondani
Alitakiwa kusimama kama kiongozi kwenye eneo la ulinzi lakini hakuwa bora sana na muda mwingi walikuwa wakiingiliana na Dante. Kizuri kwake ni aggressiveness kwenye man to man defense. Kukosa penati muhimu ya kwanza kwenye derby kunamtolea credits. Anapata alama 4/10.
6. Pappy Tshishimbi
Ni mechi ya kwanza kwa kiungo huyu mkabaji wa Yanga SC aliesajiliwa kutokea Mbabane Swallows ya Swaziland . Kwa kiasi kikubwa ndio alikuwa akifunja mipango yote ya Simba eneo la kati . Ameonesha mchezo mzuri kwenye mechi yake ya kwanza na Yanga . Aliweza kuwalinda vyema walinzi wa kati , kujenga muunganiko mzuri na kiungo wa juu Kamusoko pia kuwachezesha Ajibu na switching za kulia na kushoto kwa Martin na Rafael Daudi. Huyu anapata alama 9/10.
7. Rafael Daudi
Ni mechi yake ya kwanza ya watani wa jadi akitokea Mbeya City. Alikuwa bora kwenye kusaidia kukaba kuliko kuitembeza timu kwenye wing kwa ajili ya kushambulia kama alivyokuwa Saimoni Msuva au alivyokuwa akicheza Martin upande wa kushoto. Bado anaonekana ni mzuri zaidi kucheza kama kiungo wa kati kuliko wa pembeni. Kocha alimtoa kumuingiza Juma Abdul kuitembeza wing hiyo ambaye nae game ilimkataa na hata kukosa penati muhimu kwenye matuta. Anapata alama 5/10.
8.Thabani Kamusoko
Box to box midfielder. Alikuwa na kazi ya kusimamia mfumo wa kushambulia wa mwalimu sambamba na Ibrahimu Ajibu lakini ilimbidi kucheza double pivot kwa kushuka chini kuungana na Tshishimbi kukata dominance ya kiungo cha Simba eneo la kati hususani kuziba njia za Haruna Niyonzima kama final passer kwenye safu ya ushambuliaji. Anapata alama 7/10.
9. Ibrahimu Ajibu
Alipangwa kama " false nine " akicheza kama kiungo mshambuliaji aliyekuwa akitokea kati na pembeni kulingana na mfumo wa shambulizi au build up . Kama Ngoma angekuwa makini kwenye pressing basi wangetengeza pacha nzuri na Ajibu. Muda mwingi alionekana kukosa msaada wa kumalizia kazi yake kwa Ngoma kushindwa kukaa vyema ndani ya box . Anapata alama 7/10.
10. Donald Ngoma
Hakuwa bora kwenye kiwango chake yaonyesha bado hajawa fit baada ya kutoka kwenye majeraha ya goti. Kasi yake imepungua na battling kwenye safu ya ushambuliaji ni ndogo . Anapata 5/10
11. Emanuel Martini
Hakika anakwenda kuwa mchezaji tegemeo kwa George Lwandamina wing ya kushoto na hata kucheza kama kiungo mshambuliaji. Aliweza kumsumbua vyema Ally Shomari mlinzi wa kulia wa Simba . Ana kasi , nguvu , stamina na uwezo mzuri wa kutoa pasi zenye macho pia dribbling nzuri kujenga mashambulizi. Anapata alama 7/10
Post a Comment