DAR ES SALAAM, Tanzania -Klabu ya Simba imetangaza kuahirisha mkutano wake na waandishi wa habari uliopangwa kufanyika jana kwenye hoteli ya Ramada jijini Dar es Salaam.

Taarifa iliyotolewa kwenye ukurasa rasmi wa klabu hiyo inadai kuwa mkutano huo umeahirisha mkutano huo ambao walikuwa na lengo la kufanya pamoja na klabu ya Singida United.

Tunaelewa kuwa klabu hizo mbili zilikuwa zimeitisha mkutano huo kwa ajili ya kutangaza juu ya mechi ya kirafiki kati yao ambayo ilikuwa imepangwa kuchezwa siku ya jumapili kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.

Lakini hata hivyo taarifa zaidi zinaeleza kuwa mechi hiyo imeahirishwa kutokana na maombi yao ya kutumia uwanja wa taifa kupigwa chini.

Post a Comment

 
Top