Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Walemavu), Jenista Mhagama amesema ujenzi wa uzio, makazi na ofisi binafsi ya Waziri Mkuu umekamilika.
Julai 26, mwaka huu, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alisema atahamia rasmi mjini hapa Septemba Mosi mwaka huu.
Hata hivyo, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana alisema shughuli za mapokezi yake hazitafanyika tena Septemba Mosi ili kupisha vikao vya Bunge vinavyoanza Jumanne wiki ijayo
Post a Comment