Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amepuuzia  taarifa za hivi karibuni za uvumi juu ya afya yake, kwa kusema kwamba alikufa na akafufuka.  Mugabe mwenye umri wa 92, aliyasema hayo alipokuwa akiwasili kwenye uwanja wa ndege wa Harare akitokea nje ya nchi.Taarifa ya safari yake ilisema kuwa ndege yake ilikuwa ikielekea mashariki mwa Asia, na kwamba badala yake ilikwenda Dubai. Mwezi Mei, Mke wa Mugabe, Grace, alisema kuwa mumewe ataongoza nchi hata akiwa kaburini. Raisi huyo ameendelea na vituko vyake pamoja na kauli zake tata ambazo ushangaza ulimwengu.



Post a Comment

 
Top