Maendeleo ya Afrika yatakuwa ni moja kati ya ajenda muhimu zikazojadiliwa kwenye mkutano wa kundi la nchi 20 utakaofanyika mwanzoni mwa mwezi ujao mjini Hangzhou, Mashariki mwa China.
Wakiongea mjini Beijing kwenye kongomano la wanahabari na wataalam wa ushirikiano wa kimataifa, wataalam mbalimbali wamesema China inaichukulia ajenda ya maendeleo ya Afrika kwa umuhimu mkubwa, na imezialika Chad, Senegal na Misri kuziwakilisha nchi za Afrika kwenye mkutano huo.
Mtafiti mwandamizi wa taasisi ya mambo ya Asia Magharibi na Afrika wa Chuo Kikuu cha Peking Profesa Liu Naiya, amesema maendeleo ya Afrika, na hasa maendeleo ya viwanda na manufaa yake kwa nchi za Afrika, yatajadiliwa kwenye mkutano huo. Amesema kuwekwa kwa ajenda hiyo, na ushiriki wa nchi za Afrika kwenye mkutano, kunaonesha jinsi China inavyouchukulia kwa umuhimu mkubwa maendeleo ya Afrika.
Mtafiti kwenye kituo cha masuala ya zama hizi cha idara ya kimataifa ya chama cha kikomunisti cha China Bw Zhao Minghao, amesema mbali na maendeleo ya viwanda, mkutano wa Hangzhou pia utajadili namna ya kukabiliana na changamoto za usalama wa chakula na mabadiliko ya hali ya hewa kwa bara la Afrika, na hatua za utekelezaji kwenye kufikia malengo ya maendeleo kuelekea mwaka 2030.
Home
»
»Unlabelled
» Maendeleo ya Afrika kuwa moja ya ajenda muhimu kwenye mkutano wa G20 utaokafanyika Hangzhou, China
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment